Tutahakikisha usalama wa fedha zako

CardeaPage inakupa njia salama kukuwezesha kununua gari la ndoto zako.
Tutazishikilia pesa zako hadi pale itakapothibitishwa kuwa gari lako litasafirishwa.

Faida tatu za CardealPage

1. Je, ni mara ya kwanza kwako kununua gari kutoka kwa muuzaji? Usiwe na shaka!

Kwa kutumia CardealPage, hautatuma fedha yako kwa muuzaji bali kwenye akaunti ya CardealPage na sisi tutazituma fedha zako kwa muuzaji mara tu baada ya kuona uthibitisho kuwa gari lako limesafirishwa.
Hivyo, tutakuhakikishia kuwa utalipokea gari lako.

CardealPage inapigiwa chapuo na kiwango kikubwa cha magari tunayouza yapatayo 2,000 kwa mwaka. Mteja wetu upo kwenye mikono salama!

2. Ukaguzi kabla ya gari kusafirishwa.

Pia utaweza kuchagua huduma yetu ya "Cardeal Inspection" kama huduma ya ziada, ambapo mkaguzi wetu atakwenda moja kwa moja kulinganisha taarifa za gari kama mlivyokubaliana wakati wa kununua. Mkaguzi ataangazia hali ya gari na sifa zilizoaijnishwa kabla ya gari kusafirishwa.

Tafadhali bonyeza linki iliyopo hapo chini kwa taarifa zaidi.
Nini maana ya "Cardeal Inspection?

3. Hakikisho la pesa itakayorejeshwa!

Iwapo muuzaji atashindwa kusafirisha gari yako, fedha zako zilizohifadhiwa na CardealPage zitarejeshwa!

Cardeal Inspection

Nini maana ya "Cardeal Inspection?

"Cardeal Inspection" huhakikisha ya kwamba unapata gari lako na maelezo yanayofanana kama mlivyokubaliana wakati wa ununuzi.
Mkaguzi wa CardealPage atadadisi kwa marejeo mtambuko ili kupata maelezo zaidi ya gari kusafirishwa.
Huduma hii inachaguliwa kama chaguo la ziada.

"Cardeal Inspection" inagharimu $150 kwa kila muamala.

US$ 150

Hujafurahishwa na hitilafu zilizopatikana? Hakuna wasiwasi! Una hakikisho ya kurejeshewa fedha!

CardealPage itakujulisha ikiwa kuna hitilafu zilizopatikana kutokana na ukaguzi.
Basi utapewa fursa za kutatua tofauti hizo na mwuzaji, au kurejeshewa fedha.

* Ikiwa haitapita "Cardeal Inspection" na unachagua urejeshewe pesa, utarudishiwa pesa zote ulizolipa lakini ada ya "Cardeal Inspection" itaondolewa.

ZAIDI, utatumiwa picha za gari lako kutoka kwa ukaguzi!

We will take picture(s) of your vehicle from Cardeal Check and send them to you.
Unaweza kuchukua faraja kwa kuona hasa gari lako linavyoonekana kabla ya kusafirishwa kwa meli!

*Upatikanaji wa huduma hii unategemea utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa vitu kwenye bandari. Hatuwezi kuthibitisha huduma hii kila wakati.

Tunakagua ili kutathmini kama kuna Udanganyifu wa Mita!

Miongoni mwa magari ya Kijapani ambayo unataka kuagiza, kunaweza kuwa na gari yenye udanganyifu wa mita (umbali bandia). Pia, baadhi ya wauzaji wa nje hufanya udanganyifu wa mita wakati wanapouza magari.
Wakati wa Ukaguzi wa CardealPage, mekanika pia ataangalia gari kutathmini ikiwa kuna udanganyifu wa mita umefanywa au la.
Ikiwa mekanika amegundua ya kuwa kuna udanganyifu wa mita, tutakujulisha. (Itakuwa kwa magari yaliyo na historia ya mauzo kwa mnada iliyofanyika zamani).


Hati ya Uthibitishaji ya Odometa

Vitu vya kukaguliwa na Cardeal

Chini hapa ni vitu vya kukaguliwa na Cardeal.

Vitu vya kukaguliwa
<Vipimo kamili>
Jina la Gari Sharti liorodheshwe.
Msimbo wa Modeli
Namba ya Chesisi
Umbali kwa maili
1. Tofauti ya umbali wa maili kati ya kilomita 1,000 kwa upande wowote inakubaliwa.
2. Odometa imerudishwa nyuma: ndiyo/hapana (tutaangalia kama umbali wa maili umerudishwa nyuma kwa kufuatilia historia ya umbali wa maili).
3. Odometa umebadilishwa: ndiyo/hapana.
Msimbo wa Injini Inapaswa kuwa sawa na kama ilivyoonyeshwa kwenye Kibali cha Kuuza Bidhaa Nje..
Mwaka / Mwezi wa Usajili
Mwaka wa Mkanda wa Usalama wa Kiti Sharti liorodheshwe.
Aina ya Petroli
Saizi/Ukubwa ya/wa Injini
Aina ya Giaboksi
Aina ya Gari (2WD/4WD)
Namba ya Milango
Idadi ya Viti
Rangi
Usukani
<Vifaa>
Mfumo wa kiyoyozi cha gari Halali ikiwa vipengele vyote kama gesi na kishinikizi vinafanya kazi kama inavyotarajiwa, na hutoa hewa baridi.
Usukani unaotumia Umeme Halali ikiwa Usukani unaotumia Umeme unafanya kazi kama kawaida/inavyotarajia.
Madirisha yanayotumia Umeme Halalai ikiwa Madirisha yanayotumia Umeme yanafanya kazi.
Breki za ABS Halali ikiwa gari lina breki za ABS, na kwamba taa la onyo la breki hizo haliwaki kwa dashibodi.
Mfuko wa Hewa Halali ikiwa lina Mfuko wa Hewa, na kwamba taa la onyo haliwaki kwa dashibodi.
Vioo vinavyotumia Umeme Halali ikiwa pembe zinaweza kurekebishwa upande wa kushoto/kulia kwa amri.
Ufunguo wa Kati ya Kielektroniki Halali ikiwa milango yote yanafungwa kwa amri kupitia swichi iliyoko upande wa dereva.
Yasiyo na Funguo Halali ikiwa gari inaweza kufungwa/kufunguliwa na kifaa hiki.
Redio ya Kaseti Halali ikiwa inacheza muziki kwa amri.
Redio ya CD
CD Changer
Paa linaloweza kufunguka Halali ikiwa kuna dirisha kwa paa, na inasonga kwa amri.
Kiti cha Ngozi Halali ikiwa sehemu yoyote ya kiti ni ngozi.
<Kisanduku kilichojazwa na vifaa>
Jeki Sharti liwe na seti kamili ya sehemu zinazohitajika kuinua gari ili kustahili kama "Jeki".
Kisanduku cha vifaa Sharti liwe na seti kamili ya sehemu zinazohitajika kubadilisha magurudumu ili kustahili kama "Kisanduku cha vifaa".
Gurudumu la Akiba Haipaswi kuwa na pancha ili listahili kama "Gurudumu la Akiba".
Ufunguo wa Akiba Inapaswa kuwasha injini na pia kuweza kufunga/kufungua mlango ili kustahili kama "Ufunguo wa Akiba".
<Hali>
Injini Halali ikiwa hakuna sauti isiyo ya kawaida, na uvujaji wa mafuta ambayo inaweza kuleta matatizo ya kuendesha gari wakati injini imewashwa.
Gesi ya Eksozi Halali ikiwa hakuna moshi nyeupe/nyeusi.
Giaboksi Halali ikiwa hakuna mshtuko wa kuhama au kuteleza na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuleta matatizo ya kuendesha gari.
Rejeta Halali ikiwa hakuna uvujaji wa mafuta ambayo inaweza kuleta matatizo kwenye gari lako.
Harufu ya Ndani Halali ikiwa hakuna harufu ya sigara, kipenzi, na kitu kingine chochote kisichofaa.
Kioo cha mbele cha gari Halali ikiwa hakuna nyufa nyingi zaidi ya 1.5cm kwa urefu / kipenyo.
Taa la Onyo Halali ikiwa hakuna taa la onyo linawaka kwenye dashibodi.
Taarifa ya Ziada
SIO Halali kama gari linapatikana na matatizo yafuatayo, bila maelezo zaidi katika Taarifa ya Ziada. Matatizo kwa hali ya gari, na / au vifuasi.
  • Matatizo kwa hali ya gari, na / au vifuasi.
  • - Matatizo ambayo hayawezi kuonekana kupitia picha pekee
    (k.m. kasoro kutokana na ajali za awali na majanga ya asili ambayo huathiri uendeshaji wa gari.)
  • - Magari yaliyogeuzwa hasa, au aina yoyote ya ugeuzaji kwenye mwili, mitambo, na mambo ya ndani ya gari.
  • - Mambo mengine yoyote ambayo CardealPage huamua kama tatizo au kasoro kubwa.

* Cardeal Inspection haihusishi kuendesha gari kwa madhumuni ya kuhakikisha gari liko sawa. CardealPage haiwezi kuchukua jukumu lolote la matatizo ambayo yanaweza kuonekana tu kupitia uendeshaji wa gari.
* Baadhi ya magari yameorodheshwa na maelezo mafupi. Cardeal Inspection utafanywa kwa kutumia taarifa yoyote inapatikana.